Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 04:22

DRC na Rwanda wakubaliana kuhusu M23


Pendekezo hilo liliwasilishwa na kundi la nchi za maziwa makuu linaloundwa na nchi 11

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC- na Rwanda wamekubaliana juu ya pendekezo la kuwa na kikosi cha jeshi kisichofungamana na upande wowote kwenye mpaka wao. Makubaliano hayo yalitiwa saini na marais wa nchi hizo mbili Jumapili ikielezea jeshi lililopendekezwa litasaidia kutokomeza kundi la M23 la waasi wa Congo na makundi mengine yenye silaha katika eneo.

Pendekezo hilo liliwasilishwa na kundi la nchi za maziwa makuu, linaloundwa na nchi 11 zikiwemo Rwanda, Congo na nchi nyingine za jirani.


Haijawekwa bayana nchi gani kati ya hizi zitatoa wanajeshi kwenye jeshi hilo lisilofungamana na upande wowote au fedha zitatoka wapi japokuwa Umoja wa Afrika unasema utajiandaa kusaidia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda anasema makubaliano hayo sio suluhisho lakini sehemu ya suluhisho kwa waasi wa kundi la M23 ambalo lilianza mwezi April na Rwanda inakanusha kuwasaidia.

Waasi wa kundi la M23 wanaongozwa na makamanda wa kundi la kabila la wa-Tutsi ambao kwa miaka mingi wamekuwa na ushirikiano madhubuti na serikali yenye wa-Tutsi wengi nchini Rwanda.

Kiongozi wa jumuiya ya wa-Tutsi, raia wa Congo, Edouard Mwangachuchu ameiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba makubaliano hayo ni ishara nzuri na anasema vita vya M23 vinaweza kumalizika kwa mashauriano.

Waasi wa M23 walitangaza jina lao kutoka kwenye mkataba waliotia saini na serikali ya DRC mwezi machi mwaka 2009, ambapo walikubaliana kuingia katika jeshi na kuondoa tofauti zao za kisiasa na kisha walikitaka chama cha National Congress for the Defence of the People-CNDP kuingia katika siasa.

Wanasema walianzisha kundi la uasi la M23 kwa sababu mkataba wa Machi 23 haujawahi kutekeleza ipasavyo mahitaji yao.

XS
SM
MD
LG