Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:12

DRC kupambana na homa ya manjano

Antho akimwangalia mwanae aliyelazwa hospitali huko Drc.
Antho akimwangalia mwanae aliyelazwa hospitali huko Drc.

Waziri wa afya Felix Kabange amesema kampeni hiyo itaanza rasmi julai 20 na itakuwa na lengo la kutoa chanjo kwa kila mmoja kwenye mji mkuu , Kinshasa isipokuwa kwa watoto walio chini ya miezi tisa na pia chanjo hiyo italenga kwenye majimbo ya Kwango, Lualaba, na Kasai.

Jamhuri ya kidemokrasi ya congo imesema itaanza kampeni mwezi ujao kutoa chanjo kwa watu milioni 11.6 ili kupambana na ugonjwa wa homa ya manjano baada ya mlipuko kutangazwa rasmi katika mji mkuu.

Waziri wa afya Felix Kabange amesema kampeni hiyo itaanza rasmi julai 20 na itakuwa na lengo la kutoa chanjo kwa kila mmoja kwenye mji mkuu , Kinshasa isipokuwa kwa watoto walio chini ya miezi tisa na pia chanjo hiyo italenga kwenye majimbo ya Kwango, Lualaba, na Kasai.

Wiki iliyopita serikali ya congo ilitangaza mlipuko huo katika mji wa Kinshasa na majimbo mengine mawili baada ya ripoti kuthibitishwa kuwa kuna kesi 67 za homa ya manjano na zaidi ya watu wengine elfu moja wanahisiwa kuwa na ugonjwa huo.

Mlippuko katika nchi jirani ya Angola umesababisha vifo vya watu 345. Kabange hakusema ni jinsi gani maafisa wa afya watatoa chanjo kwa watu wote .

Hivi sasa kuna upungufu wa chanjo hiyo kote duniani na inatakiwa angalau mwaka mmoja kwa ajili ya kuitengeneza. Shirika la afya duniani- WHO lilipendekeza mwezi huu kwamba ipunguziwe uwezo wake hadi kiwango cha tano cha dozi ili kukabiliana na dharura iliyopo.

XS
SM
MD
LG