Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 01:27

DRC Kuhamisha ubalozi wake nchini Israeli kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem


Rais wa DRC Felix Tshisekedi
Rais wa DRC Felix Tshisekedi

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itahamisha ubalozi wake wa Israeli hadi Jerusalem kutoka Tel Aviv, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Ijumaa.

Netanyahu, ambaye alikutana na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alitangaza katika taarifa kwamba Israeli pia itafungua ubalozi huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ni nchi chache tu zilizo na balozi zao mjini Jerusalem, huku nyingine nyingi zikidumisha uwakilishi wao wa kidiplomasia katika mji wa pwani wa Tel Aviv, kitovu kikuu cha kiuchumi cha Israeli.

Wakati Israeli inauchukulia mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wake wa milele, na uslio imara, huku ikitaka balozi zote ziwepo humo, sehemu kubwa ya dunia haitambui mamlaka ya Israeli dhidi ya mji wote wa Jerusalem, wakiamini suala hilo linapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Wapalestina wanataka watambuliwa kama taifa na mji wao mkuu uwe katika eneo la mashariki mwa Jerusalem, ambalo Israeli ililiteka katika vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967.

Forum

XS
SM
MD
LG