Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:45

DRC inatarajiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na safari


Ghasia za wafuasi wa upinzani nchini DRC
Ghasia za wafuasi wa upinzani nchini DRC

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa ulaya huko Luxembourg unatarajiwa Jumatatu kukubaliana juu ya taarifa ambayo itaweka bayana marufuku ya safari na kuzuia mali za baadhi ya maafisa wa serikali wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC ni kitisho cha kweli ikiwa uchaguzi mkuu hautafanyika kati ya mwaka huu na mapema mwaka 2017.

Wanadiplomasia wanasema umoja wa ulaya utatangaza vikwazo vya kiuchumi kwa DRC endapo muungano unaotawala nchini humo hautatayarisha uchaguzi mpya baada ya uchaguzi wa mwezi ujao kucheleweshwa.

Rais Joseph Kabila wa DRC alitarajiwa kumaliza muda wake madarakani mwishoni mwa mwaka huu hapo Disemba lakini maafisa wa tume ya uchaguzi nchini humo waliakhirisha uchaguzi mkuu hadi April mwaka 2018 wakieleza kutokana na sababu za kiufundi zilizojitokeza.

XS
SM
MD
LG