Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 21:16

DRC inajitayarisha kwa uchaguzi baada ya ghasia Kinshasa


DRC inajitayarisha kwa uchaguzi baada ya ghasia Kinshasa
DRC inajitayarisha kwa uchaguzi baada ya ghasia Kinshasa

Wapiga kura wa DRC wanajitayarisha kwa uchaguzi mkuu Jumatatu, huku wagombea wa upinzani wakidai wizi wa kura.

Viongozi wa upinzani wanailaumu serikali kwa kusababisha ghasia zilizozuka Jumamosi mjini Kinshasa, ili kuweza kupanga wizi wa kura.

Makamu rais wa tume ya uchaguzi Jacques Djoli Eseng'Ekeli, anasema masanduku ya kura na karatasi za upigaji kura zinasafirishwa kwa helikopta hadi vituo vya mbali vya upigaji kura katika taifa hilo lenye ukubwa wa Ulaya Magharibi.

Eseng'Ekeli anasema kutakuwa na matatizo kwa baadhi ya watu kuweza kujuwa mahali ya kupigia kura, lakini anatarajia kwamba kila mtu hatimae ataweza kupiga kura yake.

Katika uchaguzi huu wa pili wa vyama vingi tangu uhuru wa DRC, na wa kwanza kupangwa na wa-Kongo wenyewe, unakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa na uchukuzi.

Kukiwa kuna zaidi ya watu elfu 18 wanaogombania viti 500 vya bunge, basi wapiga kura katika baadhi ya vituo vya kupiga kura katika mji mkuu wapigaji kura huwenda wakapewa zaidi ya kurasa 50 za vyeti vya kupiga kura.

XS
SM
MD
LG