Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 03:41

DRC yatangaza bajeti dola milioni saba


Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza bajeti yake mpya ambayo ina ongezeko kubwa la matumizi kwa mwaka 2011.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza bajeti yake mpya ambayo ina ongezeko kubwa la matumizi kwa mwaka 2011.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Adolphe Muzito aliwasilisha bungeni mswada wa bajeti ya serikali.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa Alhamisi imefikia dola bilioni saba, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zinatarajiwa kutolewa na wafadhili wa Congo. Hii ni mara ya kwanza tangu nchi ya Congo ijipatie uhuru wake kuwasilisha bajeti yenye kiwango cha juu kama hicho. Lakini wataalam wa maswala ya uchumi nchi humo wanasema licha ya bajeti kubwa namna hiyo bado hali ya maisha kwa raia wa kawaida nchini humo ni duni.

Waziri wa Fedha Jean Baptiste Nthawa Kuderwa amesema kuwa bajeti hiyo pia inajumuisha fedha kwa matayarisho ya uchaguzi mwakani.

XS
SM
MD
LG