Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:39

Rais wa zamani wa Angola Dos Santos mahututi hospitali, Bercelona


Rais wa zamani wa Angola Eduardo Dos Santos aliyeinua mkono juu kwenye picha ya zamani.
Rais wa zamani wa Angola Eduardo Dos Santos aliyeinua mkono juu kwenye picha ya zamani.

Shirika la habari la Ureno LUSA limeripoti Ijumaa kuwa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, yuko katika hali mahtuti kwenye hospitali moja mjini Barcelona, Uhispania.

Dos Santos alitawala taifa hilo la pili lenye utajiri wa mafuta barani Afrika kwa miongo takriban minne.
Dos Santos mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akipokea matibabu tangu mwaka 2019, lakini afya yake imezidi kuzorota na hivyo kuhamishwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Serikali ya Angola bado haijajibu hadi sasa kuhusu ya hali ya afya ya kiongozi huyo wa zamani .
Dos Santos ni mojawapo wa viongozi waliotawala kwa mda mrefu barani Afrika, alistaafu miaka mitano iliyopita. Uongozi wake uligubikwa na vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea kwa takriban miono mitatu baina ya serikali na kundi la waasi walioungwa mkono na Marekani la UNITA.

Baina ya miaka 2002 na 2014, pale uzalishaji mafuta ulipoongezeka na bei ya mafuta kupanda, uchumi wa Angola ulipanuka zaidi kutoka billioni 12.4 hadi billioni 126 dola. Lakini utajiri huo haukutiririka kwa watu masikini, ila wale walokuwa karibu zaidi na rais Dos Santos walizidi kutajirika. i

XS
SM
MD
LG