Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:16

Seneta John McCain ampinga Donald Trump


Donald Trump speaks akizungumza kwenye mkuutano wa kampeni huko Colorado Springs, Colo. , Julai 29, 2016.
Donald Trump speaks akizungumza kwenye mkuutano wa kampeni huko Colorado Springs, Colo. , Julai 29, 2016.

Staili ya Donald Trump ya kuongea bila kujali anachosema ilimsaidia kupata uteuzi wa chama cha Republikan kugombea urais lakini ukosoaji wake kuhusu familia ya mwanajeshi wa Marekani aliyeuwawa Iraq umeleta shutuma kutoka kwa maafisa wa chama hicho na makundi ya wanajeshi wa zamani.

Seneta John McCain amesema anapingana kwa kiasi kikubwa na maneno hayo ya Trump kuhusiana na mwanajeshi Humayon Khan kwamba watu walio na imani kama yake wasiruhusiwe kuingia nchini Marekani.

“Natumaini wamarekani wataelewa kwamba maneno haya hayawakilishi mawazo ya chama cha Republikan, au wagombea McCain alisema. “wakati umefika kwa Donald kuweka mfano nchin kwetu na siku zijazo za chama cha Republikan, Wakati chama chetu kimemchagua hayo hayaji na leseni ya kutukana wale walio bora kati yetu.

XS
SM
MD
LG