Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 23:20

Trump aelekea kupata uteuzi wa Republikan kugombea urais


Mgombea urais wa Republican, Donald Trump akiwasili kwenye mkutano wa kampeni baada ya kushinda uchaguzi wa awali katika jimbo la Indiana.

Mfanyabiashara bilionea Donald Trump sasa ndiye mgombea mtarajiwa kwa tikiti ya chama cha Republican kwenye uchaguzi wa rais. Hata hivyo ishara za mapema zinaonyesha kwamba anakabiliana na kibarua kigumu dhidi ya anayetarajiwa kuwa mgombea wa tikiti ya chama ca Democratic, Hillary Clinton.

Ukusanyaji maoni uliofanywa na vyombo mbali mbali unaonyesha Clinton, ambaye ananuia kuwa rais wa kwanza mwanamke hapa Marekani, akimshinda Trump, ambaye aliibuka mshindi katika uwanja uliokuwa na washindani wengi, kwa kuwa na msimamo mkali kuhusu wahamiaji haramu kutoka Mexico na kuwazuia kwa muda Waislamu walionuia kuingia nchini.

Kwa ujumla ukusanyaji huo wa maoni unamuonyesha Bi Clinton, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani kati ya mwaka wa 2009 na 2013, akimshinda Trump, ambaye hajawahi kushikilia nafasi yoyote ya kuchaguliwa, kwa asili mia sita.

XS
SM
MD
LG