Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 22:47

Dominique Strauss-Kahn arejea Ufaransa


Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn na mkewe Anne Sinclair mjini New York July 1, 2011.
Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn na mkewe Anne Sinclair mjini New York July 1, 2011.

Mkuu wa zamani wa shirika la IMF arejea nchini mwake

Mkuu wa zamani wa shirika la kimataifa la fedha ( IMF) Dominique Strauss-Kahn amereja nchini mwake Ufaransa mapema Jumapili. Yeye na mkewe Anne Sinclair waliwasili Ufaransa kwa ndege ya shirika la Air France kutoka New York. Strauss -Kahn alijiuzulu kama mkuu wa shirika la IMF mwezi Mei mwaka huu baada ya kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Kennedy na kushtikiwa kwa makosa ya ngono na jaribio la kumbaka mhudumu wa hoteli moja mjini New York. Alifungwa jela kwa takriban wiki moja na kisha kutumika kifungo cha nyumbani kwa wiki sita na kuzuiwa kuondoka nchini Marekani. Lakini wiki jana aliachiwa huru baada ya waendesha mashitaka katika mahakama yamoja mjini Manhattan kutupilia mbali kesi dhidi yake wakisema wasingeweza tena kumwamini Nafissatou Diallo, mhamiaji kutoka Guinea aliyemshtaki kwa makosa ya ngono. Strauss- Kahn alitazamiwa kuwa mpinzani mkuu wa rais Nicolas Sarkozy katika uchaguzi wa urais mwaka wa 2012 kabla ya kupata pigo hilo la kashfa ya ngono.

XS
SM
MD
LG