Uharibifu huo umepelekea kukatika kwa huduma ya umeme na maji kwa mamilioni ya watu wa Ukraine huku msimu wa baridi kali ukiwa umeanza.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna amesema kwamba pesa hizo zimetolewa kutoka kwa wahisani wapya na kwa nia njema na waa sio mkopo.
Amesema kwamba msaada huo utaanza kutumika katika muda wa siku chache zijazo ili kuimarisha mifumo muhimu.
Karibu dola milioni 400 zitatumika kutengeneza mfumo wa nshati wa Ukraine ambao Russia imekuwa ikilenga zaidi kwa makombora.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliambia viongozi wa G7 kwamba nchi yake ilihitaji msaada wa kifedha usiopungua dola milioni 840.