Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:39

Rais Magufuli aahidi kupambana na mafisadi ndani ya CCM


Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais wa Tanzania, John Magufuli

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Rais John Magufuli, ameapa kupambana na mafisadi ndani ya chama hicho ambao amesema wamekuwa wakikwamisha maendeleo ya chama kwa kipindi kirefu

Mwenyekiti huyo wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , John Magufuli alikuwa akizungumza kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam Ijumaa ambako amepokelewa rasmi kichama tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma hivi karibuni

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Amesema CCM kupitia jumuiya zake kama Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), umoja wa vijana (UVCCM) na jumuiya ya wazazi ina vitega uchumi vingi ambavyo vingefanya chama hicho tawala kutokumbatia wafanyabiashara kwa kuomba misaada ya fedha wakati wa kufanya chaguzi mbalimbali lakini baadhi ya viongozi na wanachama wamekuwa wakijinufaisha kupitia vitega uchumi hivyo.

Mwenyekiti huyo wa CCM taifa amesisitiza nia ya serikali yake yote kuhamia Dodoma kabla ya kumaliza kipindi chake cha Urais cha miaka mitano kwa kuwa amechoshwa na michakato isiyokwisha.

Magufuli amepokea uenyekiti wa CCM taifa toka kwa mtangulizi wake rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Dodoma ambapo ndiko alitangaza azma ya serikali yake kuhamishia shughuli zake mkoani humo

XS
SM
MD
LG