Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 09:28

DNC: Walz awaeleza wafuasi wake jinsi watakavyo pambana kushinda uchaguzi

Mgombea nafasi ya makamu wa rais Tim Walz akihutubia Mkutano mkuu wa Demokratik Chicago, Illinois, Jumatano, Agosti 21, 2024.
Mgombea nafasi ya makamu wa rais Tim Walz akihutubia Mkutano mkuu wa Demokratik Chicago, Illinois, Jumatano, Agosti 21, 2024.

Gavana wa Minnesota Tim Walz Jumatano usiku amekubali rasmi uteuzi wa chama chake kugombea nafasi ya makamu wa rais.

Gavana wa Minnesota Tim Walz Jumatano usiku amekubali rasmi uteuzi wa chama chake kugombea nafasi ya makamu wa rais.

Mgombea wa makamu wa urais alitumia hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa Demokratik kuwashukuru wajumbe waliofurika katika ukumbi kwa “kuleta furaha” katika uchaguzi uliobadilika kwa kumpa nafasi ya juu kuwa mgombea mwenza wake Makamu wa Rais Kamala Harris.

Mgombea urais Kamala Harris akiwa na mgombea mwenza wake Tim Walz wakati wa kampeni huko Milwaukee, Wisconsin, Agosti 20, 2024. (Pho
Mgombea urais Kamala Harris akiwa na mgombea mwenza wake Tim Walz wakati wa kampeni huko Milwaukee, Wisconsin, Agosti 20, 2024. (Pho

Sijatoa hotuba nyingi kubwa kama hii, lakini nimekuwa nikizungumza mara nyingi.

Wademokrat walikusanyika katika ukumbi wa Chicago, United Center wakitumaini kujenga uchachamavu aliouleta Harris tangu kuchukua nafasi ya juu ya chama ya kugombea urais mwezi uliopita.

Wanataka kutumia furaha ya Demokratik iliyokuja baada ya Rais Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais huku akiwaambia wafuasi wake kuwa wanakabiliwa na ushindani mkali dhidi ya Rais wa zamani Donald Trump.

Wamarekani wengi walikuwa hawajawahi kumsikia Walz mpaka Harris alipomfanya kuwa mgombea mwenza. Katika wiki za awali za kampeni, amewavutia wafuasi wake kutokana na uzoefu wake na alisaidia kuleta uwiano kwa uzoefu wa Harris wa mwambao kama uwakilishi wa kitamaduni wa majimbo ya Magharibikati ambao kura zao anazihitaji katika kipindi hiki.

Forum

XS
SM
MD
LG