Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:14

Dlamini-Zuma hatowania tena uenyekiti wa AU


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma.

Mkutano wa 27 wa Umoja wa Afrika umefunguliwa mjini Kigali nchini Rwanda kwa kauli mbiu “2016: mwaka wa haki za binadamu” na kulenga mahususi juu ya haki za wanawake.

Mkutano wa wakuu wa nchi utafanyika Julai 17 na 18. Masuala mengine muhimu kwenye ajenda ya mkutano huo ni ukweli kwamba mwenyekiti wa sasa wa AU Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika kusini ameamua kutowania muhula wa pili. Kuna uvumi kwamba Botswana, Equatorial Guinea na Uganda zitaweka majina ya mawaziri wao wa mambo ya nje ili kuchukua nafasi ya bibi Dlamini-Zuma.

Lakini Chika Onyeani, mhariri mkuu wa gazeti la African Sun Times anasema inabidi kuwepo na kipimo cha kiwango cha demokrasia katika nchi ambazo wagombea wake wanawania kuchukua nafasi ya bibi. Dlamini-Zuma. Alisema viongozi wanaotumia nguvu kuwatawala watu wao hawatakiwa kupewa nafasi ya uwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG