Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 11:26

Hussein Mwinyi apitishwa kugombea urais Zanzibar 2020


Dkt Hussen Mwinyi

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kimempitisha Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi kugombea urais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Ijumaa na Chama hicho mchakato unaofuatia ni Jina la mgombea huyu litafikishwa katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ili kumthibitisha rasmi kuwa mgombea wa CCM Zanzibar.

Dkt Mwinyi amepata kura 129 katika kura za mchujo ambazo ni asilimia 78 ya kura zote.

Wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho akiwemo Shamsi Vua Nahodha aliyepata kura 16 na Dkt Khalid Salim Mohammed aliyepata kura 19.

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kutangazwa mshindi na kupewa ridhaa ya kugombea urais wa Zanzibar, Mwinyi amesisitiza ushirikiano na mshikamano ndani ya chama hicho wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2020.

Amesema ushirikiano na mshikamano ndiyo utakao kiwezesha chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwa pande zote mbili za muungano.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG