Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:01

Dini yachukuwa nafasi ya juu kwenye uchaguzi Brazil


Wagombea wa urais nchini Brazil, kabla ya mdahalo mjini Sao Paulo, Octoba 16, 2022.
Wagombea wa urais nchini Brazil, kabla ya mdahalo mjini Sao Paulo, Octoba 16, 2022.

Dini ina umuhimu mkubwa katika siasa za Brazil, ambako takriban aslimia 59 ya watu huko wanasema ni kigezo muhimu kwa jinsi wanavyopiga kura, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni uliofanywa na kampuni ya Datafolha.
Taifa hilo la Amerika Kusini lina wakazi takriban milioni 215, nalo lina idadi kubwa sana ya waumini wa kikatoliki. Takriban nusu ya wakazi ni wakatoliki, na pia Brazil ina jumuiya kubwa inayoongezeka ya waumini wa kiinjilisti, ambao ni takriban theluthi moja ya wapiga kura.
Rais Bolsonaro ambaye ni mkatoliki amejenga uhusiano wa karibu na wainjilisti, na kufanya dini ni kiini cha kampeni yake, yenye kauli mbiu inayosema: "Mungu, taifa, familia na uhuru."
Naye rais wa zamani wa Brazil ambaye pia ni mgombea wa upinzani dhidi ya Bolsinaro, Bw Lula da Silva, yeye ni muumini wa kikatoliki, lakini aghlabu huwa hazungumzii sana kuhusu imani yake, lakini sasa amekuwa akizidisha kauli juu ya dini, nakupinga habari potofu zinazomtuhumu kuwa ana njama za kufunga makanisa na hofu za wainjilisti kuhusu utoaji mimba na itikadi za kijinsia.
Lakini Lula mwenye umri wa miaka 77 amesimama kidete. Kiongozi huyo wa zamani ambaye alikuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi, anaonekana kuwa na umaarufu mkubwa kuliko rais Bolsanaro miongoni mwa wakatoliki kwa aslimia 57 kwa 37 ya rais Bolsanaro. Hata hivyo Lula anajitahidi kupata uungaji mkono zaidi miongoni mwa waumini wa kiinjilisti.

Brazil
Brazil

Lula alilazimika kubadili matamshi yake hapo mwezi Aprili, aliposema kuwa utoaji mimba ni sawa. Kauli hiyo ilizua maoni mengi kwenye taifa ambalo takriban aslimia 70 ya raia wanapinga utoaji mimba, hiyo ni kwa mujib wa maoni ya kura za maoni.
Kadhalika Lula amepambana na maelezo potofu yaliyosambaa kutoka kwa wafuasi wa rais Bolsanaro, ambao waliandika mitandaoni kumtuhumu Lula kwa dhambi, na kwamba ana njama za kufunga makanisa na kuwa anashirikiana na shetani.
Naye rais Bolsanaro ambaye anaonekana kuwa nyuma kidogo mionogoni mwa takwimu za wapiga kura, ana uhusiano wa karibu na wainjilisti. Bolsanaro anaongoza miongoni mwa wainjilisti kwa aslimia 63 dhidi ya Lula mwenye aslimia 31 miongoni mwa waumini hao.
Mkewe Bolsanaro Michelle, anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa wainjilisti, amekuwa akitembea nchini kote kumpigia debe mumewe. Ameutaja uchaguzi huu kuwa ni vita vya imani. Akisema ni vita vya uzuri dhidi ya uovu, na kumwita Lula shetani.
Mchambuzi wa kisiasa Adriano Laureno anasema kuwa Bolsanaro ameweza kufanya kampeni nzuri kwa kulifanya suala la dini kuwa ni suala kuu katika kampeni yake. Adriano anasema, ikiwa tunazungumzai suala la uchumi badala yake, basi Lula huenda yuko katika nafasi nzuri zaidi.
Tangu kumalizika duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Oktoba 2, ambapo Lula alipata aslimia 48 ya kura dhidi ya 41 za Bolsanaro, ameapa kupambana moto kwa moto na mpinzani wake. Wakitumia mitandao ya kijamii, washirika wa Lula wamekuwa wakiweka habari zinazomhusisha Bolsanaro na masuala ya kishetani na ya kifreemason.
Lula alisema kuwa serikali yake haitopigana kamwe dhidi ya uhuru wa dini, na kuwahakikishia raia kuwa anapinga utoaji mimba, suala ambalo limepigwa marufuku nchini Brazil, ila kwa kesi zinazohusiana na ubakaji, kujamiana au iwapo maisha ya mama yapo hatarini.
Mkutano wa kitaifa wa mabishop wa kikatoliki nchini humo, wametoa taarifa za kulaani wale wanaotumia imani za kidini za watu kushinda kura.

Taarifa hii imetaarishwa kutokana na ripoti za AFP

XS
SM
MD
LG