Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:16

Diktekta "Baby Doc"-Duvalier arudi Haiti


Dikteta wa zamani wa Haiti Jean-Claude "Baby Doc" Duvalier akizungumza kwa simu akiwa karibu na mkewe Veronique Roy walipowasili Port-au-Prince, Haiti, Jumapili, Jan. 16, 2011.
Dikteta wa zamani wa Haiti Jean-Claude "Baby Doc" Duvalier akizungumza kwa simu akiwa karibu na mkewe Veronique Roy walipowasili Port-au-Prince, Haiti, Jumapili, Jan. 16, 2011.

Diktekta wa zamani wa Haiti Jean-Claude Duvalier,amerudi nyumbani kwa mara ya kwanza tangu alipopinduliwa kutoka madarakani mwaka 1986.

Hadi mapinduzi, Duvalier, akijulikana kama “Baby Doc” aliiongoza Haiti tangu kifo cha baba yake mwaka 1971, Francois “Papa Doc” Duvalier.Haijulikani wazi kwa nini Duvalier mdogo alirudi.Na kurudi kwake kumetokea wakati wa matatizo ya kisiasa huko Haiti,kufuatia uchaguzi wa rais na wabunge wa Novemba 28,ambapo matokeo ya awali yamezusha shutuma za wizi wa kura na mandamano.

Uchaguzi ulifuatiwa na mlipuko wa kipindupindu katika taifa hilo la Caribbean ambalo bado linaponya kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka mmoja uliopita ambalo liliuwa zaidi ya watu 300,000. Duvalier alikuwa akiishi Ufaransa kabla ya kurudi tena Haiti.


XS
SM
MD
LG