Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 15:11

Dhoruba yatikisa jimbo la California , Marekani


Mtu mmoja akitembea katika mtaa wakati hali ya theruji imetanda Marekani

Tangu mwishoni wa Decemba dhoruba kadhaa zimeuwa takriban watu 19. Huduma za dharura za California ziliamuru watu 6,000 kuondolewa ijumaa wakati wengine takriban 20,000 walikuwa hawana umeme.

Athari za dhoruba hizi zimekuwa kubwa , Nancy Ward mkurugenzi wa ofisi ya Gavana wa California ya huduma ya dharura alisema katika Mkutano na waandishi wa habari.

Amesema tayari hadi sasa wameshuhudia dhoruba kubwa katika jimbo hilo ambazo zimefanya uharibifu na bado kuna nyingine zipo njiani kuja. Dhoruba zinaendelea kuwa hatari katika jumuiya kote California .

Kumekuwa na mafuriko, uharibifu wa nyumba huku majani ya miti yakitanda kwenye barabara na maporomoko ya matope. Kwa kuwa mvua kubwa tayari zimenyesha hali hiyo inaongeza ukubwa wa tatizo.

Hata hivyo hali ya mvua na kudondoka theruji kunakotarajiwa kutapelekea hali kuwa mbaya zaidi, na Ward ameonya kwamba ni vyema wakaazi wakachukua tahadhari zaidi.

Katika siku 18 zilizopita jimbo lililokumbwa na ukame limekuwa na wastani baada ya kupata mvua ya zaidi ya inchi tisa kwa siku kiasi ambacho kimepelekea baadhi ya maeneo kufikisha wastani wa mvua za kila mwaka, alisema David Lawrence mtaalamu wa hali

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG