Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 01:43

Dhoruba ya vumbi kukumba nusu ya Cameroon


Wanajeshi wa Cameroon wakiwa wameshika katika mazingira yenye vumbi

Waziri wa uchukuzi wa Cameroon amesema kwamba kiwango kikubwa cha vumbi kutoka jangwa la Sahara kinatarajiwa kuathiri nusu ya Cameroon.

Waziri Ernest Ngalle Bibehe, ameonya kwamba vumbi hilo linaweza kusababisha ajali za barabarani kutokana na kupunguza uwezo wa madereva kuona mbali.

Taarifa ya waziri huyo imeonya kwamba vumbi hilo linaweza pia kusababisha matatizo ya kupumua.

Vumbi kubwa linashuhudiwa kwa sasa katika eneo la kaskazini mwa Cameroon na huenda likaathiri maeneo manne ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni.

Tahadhari imetolewa ikiwataka watu kuendesha magari kwa makini na kufunika macho pamoja na pua.

Cameroon hushuhudia kiwango kikubwa cha vumbi kutoka jangwa la sahara kila mwaka, hasa sehemu za kaskazini na kusini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG