Upatikanaji viungo

Breaking News

Dereva aua mtu mmoja na kujeruhi 20 mjini New York


Dereva aua mtu mmoja na kujeruhi 20 New York.

Dereva mmoja aliendesha gari lake kiholela kwenye eneo maarufu la Times Square Alhamisi, lililo katikati ya mji wa New York na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi watu 20

Hata hivyo, tukio hilo la alhamisi alasiri majira ya pwani ya mashariki mwa Marekani, halikuaminika kuwa la kigaidi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, dereva huyo, mwenye umri wa miaka 26, aliendesha gari lake muundo wa Honda kwenye sehemu iliyokuwa na watu wengi.

Polisi walisema kuwa dereva huyo ana historia ya uendeshaji wa gari akiwa mlevi na kwamba alikamatwa huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukianza.

Kulingana na msemaji wa ikulu, Sean Spicer, Rais Donald Trump alifahamishwa kuhusu tukio hilo.

Baadaye eneo la tukio hilo lilifungwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Eneo la Times Square lina maduka na migahawa mingi na ni maarufu mno kwa watalii ambao hulitembelea kwa maelfu kila siku.

  • 16x9 Image

    BMJ Muriithi

    BMJ Muriithi is an international Broadcaster/ Multimedia specialist with Voice of America (VOA) based in Washington DC. He is a versatile journalist who has, among other assignments, covered major international events, including the UN General Assembly (UNGA) in New York, US, and the African Union Summit in Addis Ababa, Ethiopia. He also covers everyday human interest stories from around the world.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG