Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:51

Demokrasia yaporomoka katika nusu ya nchi duniani-ripoti


Ramani ya Freedom House kuhusu uhuru duniani
Ramani ya Freedom House kuhusu uhuru duniani

Nusu ya nchi za kidemokrasia duniani zinakabiliwa na kuporomoka kwa demokrasia, na hali kuwa mbaya zaidi kutokana na vita nchini Ukraine na mzozo wa kiuchumi, shirika la kimataifa la wasomi watafiti limesema Jumatano katika ripoti.

Katibu mkuu wa shirika hilo liitwalo IDEA Kevin Casas Zamora ameiambia AFP kwamba wanashuhudia kushuka vibaya kusiko kwa kawaida kwa viwango vya demokrasia hivi sasa, kukichochewa na msukosuko wa kisiasa kutokana na mzozo wa kiuchumi ulioanza na janga la Covid 19 na athari za kivita huko Ukraine.”

Idadi ya nchi ambazo viwango vya demokrasia vilishuka sana ni pamoja na Marekani tangu mwaka jana, ikiporomoka kutoka nafasi ya sita kushuka hadi nafasi ya saba mwaka huu wa 2022, nayo El Salvador ikijumuishwa kwenye orodha hiyo.

Nchi nyingine ni Brazil, Hungary, India, Mauritius na Poland.

Casas Zamora ameitaja hali ya Marekani kuwa yenye kutisha sana.

“Ninatiwa wasiwasi mkubwa na kile ninachokiona Marekani,” amesema.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, Marekani inakabiliwa na mgawanyiko wa kisiasa, taasisi ambazo hazitendi kazi ipasavyo na vitisho kwa uhuru wa raia.

XS
SM
MD
LG