Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:25

Upinzani waapa kuendelea na maandamano Kenya


Kenyan opposition supporters react and throw stones towards Kenya Police officers during demonstrations in Nairobi, Kenya on July 12, 2023.
Kenyan opposition supporters react and throw stones towards Kenya Police officers during demonstrations in Nairobi, Kenya on July 12, 2023.

Polisi wa Kenya, Jumatano walifyatua gesi ya kutoa machozi kwa waandamanaji ambao waliingia mitaani baada ya kukaidi onyo la serekali lililo tolewa mapema kuhusu maandamano yaliyo geuka ghasia ambapo watu zaidi ya dazeni waliuwawa.

Upinzani umepanga kufanya maandamano matatu kwa siku tatu mfululizo kuipinga serekali ya rais William Ruto, na kuleta wasiwasi kwa jumuiya ya kimataifa ambayo imejiunga kutoa mwito kwa suluhisho la kisiasa kutokana na mzozo huo.

Shule na maduka yalifungwa jijini Nairobi, na miji mingine, na Wakenya waliokuwa na mashaka na hali hiyo walizisihi pande zote mbili kukaa chini na kufikia muafaka.

Toka uchaguzi mkuu uliopita Kenya, imeingia katika migogoro ya kisiasa ambayo imezalisha maandamano hoja ikiwa ni ugumu wa maisha.

Forum

XS
SM
MD
LG