Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:17

Dazeni ya raia wanao jitolea jeshini Burkina Faso wauwawa


Dazeni ya raia wanaojitolea katika vikosi vya jeshi la Burkina Faso wameuwawa katika shambulio jipya kaskazini mwa nchi ambako kuna wanamgambo wenye msimamo mkali, vyanzo vya usalama na wenyeji wa eneo hilo wamesema Alhamisi. 

Kundi la kigaidi lilishambulia kikosi cha wasaidizi wa VDP Jumatano mchana karibu na Belga, takriban kilomita 170 kutoka mji mkuu Ouagadougou, vyanzo vya ndani vilisema.

Afisa wa VDP wa eneo alisema 12 walifariki dunia huku watano wakijeruhiwa, lakini akasema maadui hao pia walipata maafa.

Mwanajeshi mmoja alieleza idadi ya waliokufa kuwa ni 13, wakati VDP ilipokuwa ikifanya doria kwa kusaidiwa na jeshi dhidi ya wanamgambo.

Vifo hivyo vimeongeza idadi kutoka mashambulizi mawili wiki iliyopita katika eneo la mpaka wa kaskazini la Oudalan ambapo watu 70 waliuwawa miongoni mwao walikuwa kutoka vikosi vya usalama.

Taifa hilo lisilo na ufukwe la Sahel, linapambana na wanajihadi kutoka nchi jirani ya Mali, toka miaka minne iliyopita.

Zaidi ya raia 10,000, polisi na wanajeshi wamekufa, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserekali, huku watu milioni mbili wakikimbia makazi yao.

Takriban asilimia 40 ya eneo la taifa liko nje ya udhibiti wa serikali.

Hasira ndani ya jeshi kwa kushindwa kuleta utulivu ilisababisha mapinduzi mawili mwaka jana, na sasa limepata kiongozi wa umri wa miaka 34, Ibrahim Traore, ambaye ameapa kurejesha taifa kuwa shwari.

XS
SM
MD
LG