Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:34

Dawa za kupunguza makali ya HIV


Madawa ya kisasa yawafaa zaidi waathiriwa

Tafiti za hivi majuzi zimeonyesha kuwa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi, maarufu kama ARVs, zinaweza kutumika si kutibu virusi vya HIV tu bali pia kuzuia maambukizi. Mbinu hiyo inajulikana kwa Kiingereza kama 'pre-exposure prophylaxis' au PrEP kwa ufupi. Sasa, Jimbo la California lililo mashariki mwa Marekani linazindua tafiti mpya kukadiria uwezo wa dawa hizo kuzuia maambukizi. Tafiti hizo hazitafanyiwa katika maabara tu bali miongoni mwa watu. Tiba kama njia ya kuzuia maambukizi imefanikiwa sana katika majaribio yaliyofanyiwa katika vituo vya afya. Lakini je, itawafaa watu walio katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku? Je, watatii masharti ya kutumia dawa hata ikiwa ni kumeza tembe moja kwa siku? Haya ni baadhi ya maswali ambayo mpango wa utafiti wa California HIV/AIDS unatarajia kujibu kwa tafiti tatu mpya ambazo zitaanzishwa. Dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV zilipoanza kutumika katikati mwa miaka ya tisini, watu walilazimika kumeza tembe nyingi kila siku. Walilazimika kuzimeza saa fulani, nyakati nyingine pamoja na chakula, nyakati nyingine bila. Mara nyingi walipata madhara mabaya sana, ikiwa ni pamoja na kichefuchefu. Hata kulikuwa na visa ambapo mafuta mwilini yangejirundika nyuma ya shingo au tumboni. Kwa hivyo, huku maisha ya watu yakiokolewa,matibabu yenyewe yalisababisha wajihisi wagonjwa sana. Warren anasema hali ni tofauti sana leo. Taasisi ya Marekani ya usimamizi wa chakula na dawa – FDA itachunguza utafiti huo wa mbinu ya kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV kuzuia maambukizi ya virusi vyenyewe. Huenda uchunguzi huo ukawezesha wengi kupata dawa za kuzuia maambukizi na kuwapa wanaofanya kazi katika sekta ya afya, kampuni za bima na watu wanaotaka kutumia dawa zenyewe habari sahihi.

XS
SM
MD
LG