Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 17:38

Dawa mpya ya Covid-19 kufanyiwa majaribio


A woman holds a small bottle labeled with a "Coronavirus COVID-19 Vaccine" sticker and a medical syringe in front of displayed Pfizer logo in this illustration taken, Oct. 30, 2020.

.  Kampuni kubwa ya kutengeneza dawa ya hapa Marekani ya Pfizer imesema kwamba imeanza majaribio ya dawa inayolenga kulinda watu wanaoishi na mtu aliyeambukizwa Covid.

Dawa hiyo inalenga kuwazuia wale ambao hawana dalili zozote za maambukizi dhidi ya kupata virusi hivyo. Dawa hiyo ambayo ni ya kumezwa itafanywa majaribio kwa watu 2,660 wenye afya nzuri na ambao wameishi kwa nyumba moja na mtu aliyewahi kupata corona.

Pfizer pia inafanya majaribio ya dawa hiyo kwa watu ambao tayari walipata corona ingawa hawajaonyesha dalili zozote za maambukizi. Mkuu wa utafiti wa kisayansi kwenye kampuni hiyo Dkt Mikael Dolsten kupitia taarifa amesema kwamba iwapo dawa hiyo itafaulu, basi huenda ikadhibiti virusi vya Covid-19 kabla havijaenea zaidi.

Wakati huo huo, rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amepokea chanjo yake ya tatu maarufu kama booster muda mfupi baada ya utawala wake kuidhinisha hatua hiyo kwa makundi maalum ya watu. Muda mfupi kabla ya kupokea chanjo hiyo, Biden alisema ni muhimu kupata chanjo hiyo ya tatu lakini akahimiza kwamba lililo muhimu zaidi ni kwa watu kupokea chanjo za kwanza. Ameongeza kwamba mkewe, Jill Biden, pia atapokea chanjo hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG