Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 21:55

Darzeni  ya wahamiaji wa Afrika Magharibi wapiga kambi kwenye balozi zao nchini  Tunisia

Wanachama wa mashirika ya kutetea haki za binadamu wakiwa wamebeba mabango wakati wa maandamano, baada ya Rais Kais Saied wa Tunisia kuamuru vikosi vya usalama kuzuia uhamiaji haramu na kuwafukuza wahamiaji wote wasio na vibali, huko Tunis, Tunisia Februari 25, 2023.REUTERS

Darzeni  ya wahamiaji wa Afrika Magharibi walipiga kambi siku ya Jumanne kwenye balozi zao nchini  Tunisia baada ya kufukuzwa kutoka kwenye makazi yao, ikiwa ni matokeo ya msako wa ghafla uliotangazwa na Rais Kais Saied.

Takriban watu 50 wakiwemo watoto 11 walikuwa wamejikunyata mbele ya ubalozi wa Ivory Coast mjini Tunis, mwandishi wa AFP alisema.

Wakiwa wamejifunika na mablanketi kwa sababu ya upepo wa baridi, watu hao walisema walikuwa wamelala nje kwa siku nne.

Tunahitaji nepi na maziwa ya watoto, hatuna chakula, alisema Rokhia Kone, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Ivory Coas akiwa na mtoto wake mgongoni.

Wanaume kadhaa walionyesha vipande vya mkate vilivyopelea ambavyo walisema vingekuwa chakula chao cha pekee kwa siku hiyo.

XS
SM
MD
LG