Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:25

Tajiri Dangote kutengeneza kiwanda cha mafuta Lagos


Bill Gates,bilionea wa Microsoft, Rais Mohammadu Buhari wa Nigeria pamoja na bilionea wa Afrika Aliko Dangote. (kushoto-kulia)
Bill Gates,bilionea wa Microsoft, Rais Mohammadu Buhari wa Nigeria pamoja na bilionea wa Afrika Aliko Dangote. (kushoto-kulia)

Mpango wa kusafishia mafuta ghafi nchini Nigeria katika mji wa Lagos umekaribia kukamilika ukiwa na lengo la kumaliza upungufu wa mafuta nchini humo.

Mpango wa mtu alie tajiri kabisa katika bara la Afrika, wa kubadili sekta ya mafuta katika mojawapo ya nchi zinazozalisha bidhaa hiyo kwa wingi uko karibu kuzaa matunda nje kidogo ya mji wa kibiashara wa Lagos huko Nigeria.

Mfanyabiashara Aliko Dangote ametengeneza kiwanda cha kusafishia mafuta ghafi chenye uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kila siku ambacho ni kiasi kinachotumika kila siku nchini humo. Mara Kiwanda hicho kitakapomalizika, huenda kikamaliza tatizo la Nigeria kutegemea uagizaji wa mafuta ya taa na diseli kutoka mataifa ya nje.

Mizozo na maandamano imekuwa ikisababisha kuzuiwa kwa uagizaji mafuta na kupelekea upungufu wa bidhaa hiyo nchini. Kwa kusafishia mafuta nyumbani, Dangote amesema hilo tatizo litasahaulika. Nigeria ndio uchumi mkubwa zaidi Afrika na pia ndio nchi ilio na watu wengi zaidi barani humo.

XS
SM
MD
LG