Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:54

Dalili za covid za muda mrefu zaripotiwa Australia


Majengo ya bunge mjini Canberra, Australia
Majengo ya bunge mjini Canberra, Australia

Wakati Australia ikijiandaa kufuta  karantini ya lazima kwa wale wenye virusi vya covid-19 ifikapo Ijumaa Oktoba 14, utafiti mpya umebaini kwamba karibu theluthi moja ya watu wazima wameonyesha dalili za maambukizi kwa muda mrefu.

Kamati ya afya ya bunge mjini Canbera imesema kwamba imepata taarifa kutoka vituo vya afya kwamba kuna idadi kubwa ya watu wanaotafuta huduma za kimatibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Ripoti zimeongeza kusema kwamba licha ya viwango vya maambukizi mapya kushuka nchini humo, athari za maambukizi zimeendelea kushuhudiwa miongoni mwa baadhi ya waliomabukizwa awali.

Ripoti ya utafiti ya Jumatano kutoka chuo kikuu cha kitaifa cha Australia inaonyesha kwamba kwa kila mtu mmoja kati ya watatu waliyowahi kupata maambukizi, ameendelea kuonyesha dalili za maambukizi kwa zaidi ya wiki tatu, ikiwa ishara ya kile kimetajwa kuwa maambukizi ya Covid ya muda mrefu. Miongoni mwa dalili ni pamoja na uchovu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, maumivu ya misuli pamoja na kikohozi.

XS
SM
MD
LG