Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:55

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini amtaka rais wa Korea Kusini kukaa kimya


Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un
Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, mwenye ushawishi mkubwa Kim Yo Jong, Ijumaa amesema rais wa Korea Kusini anapaswa kufunga mdomo wake.

Ametoa kauli hii baada ya rais wa Korea Kusini kusema taifa lake lipo tayari kutoa msaada wa kiuchumi kwa Korea Kaskazini ili kuachana na silaha zake za nyuklia.

Matamshi yake yanafanya kuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa Korea Kaskazini kujibu moja kwa moja kile rais wa Korea Kusini, Toon Suk-yeol, ameuita mpango wa uthubutu ambao mara ya kwanza ulipendekezwa mwezi Mei.

Kauli hiyo ameizungumza kwa mara nyingine tena Jumatano katika mkutano na wanahabari akiadhimisha siku 100 akiwa madarakani.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari la KCNA dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini amaesema rais wa Korea Kusini ni vyema akanyamaza kuliko kuzungumza masuala yasiyo na msingi.

Waziri wa Korea Kusini anayehusika na masuala ya Korea Kaskazini amesema matamshi ya Kim hayana heshima

XS
SM
MD
LG