Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:51

Jaji ataka watuhumiwa wa CUF wafunguliwe mashitaka au waachiliwe.


Mhakama ya Tanzania kwenye picha ya awali.
Mhakama ya Tanzania kwenye picha ya awali.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mkusa Issac Sepetu, ametoa muda wa saa 24 kwa Jeshi la polisi la Zanzibar kuwasilisha sababu zinazowafanya kuendelea kuwashilikia watuhumiwa wanne wakiwemo viongozi watatu wa Chama cha Wananchi (CUF), bila ya kuwafikisha Mahakamani tangu walipokamatwa April 16 kwa tuhuma za kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jaji Mkusa ametoa agizo hilo, kufuatia ombi lililofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na Wakili anayewatetea watuhumiwa hao, Rajab Abdallah Rajab kufuatia wateja wake kuendelea kuwepo kizuizini katika kituo cha Polisi cha Mwembe Madema tangu walipokamatwa April 16, mwaka huu.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Maghrib A, Hassan Omar Issa, Katibu wa CUF Wilaya ya Maghrib A, Saleh Mohamed Saleh ambaye pia ni Mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA), Katibu wa CUF jimbo la Mfenesini Suleiman Mohamed Bakari pamoja na Omar Bakari Nassor ambao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi hilo la polisi kwa muda wa siku 20 tangu walipokamatwa. Zikiliza kwa taarifa zaidi kutoka kwa Munir Zakaria.

XS
SM
MD
LG