Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:23

Kifo cha Fidel Castro kimebainisha tofauti kubwa kati ya Obama na Trump kwa Cuba


Rais Barack Obama akiwa na rais mteule Donald Trump huko White House mapema mwezi huu.

Kifo cha rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro kumerejesha sera ya Marekani kwa Cuba kutupiwa macho tena, na kubainisha tofauti kubwa ya maoni kati rais Barack Obama na rais mteule Donald Trump.

Obama amefungua mahushiano ya Marekani na Cuba baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhusiano mbaya, hii itakuwa ni moja ya mafanikio yake ya sera zake za mambo ya nje. Amelitembelea taifa hilo la Carribean mwezi Machi akiwa ni rais wa kwanza wa Marekani aliye mamlakani kufanya hivyo tangu mwaka 1928.

“Nimekuja hapa kuzika mabaki ya mwisho ya vita baridi duniani katika bara la amerika”, aliwaelezea wananchi wa Cuba.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita, nchi hizo mbili zimefungua balozi zao baada ya zaidi ya miaka 50. Meli za Marekani hivi sasa zinatia nanga nchini Cuba, na kuna safari za ndege za mara kwa mara za mashirika ya ndege ya Marekani zinazokwenda kwenye kisiwa hicho.

Akizungumzia kifo cha Fidel Castro, Obama alitoa taarifa ya maandishi ya kidiplomasia, akituma salaam za rambi rambi kwa familia ya Castro. Taarifa hiyo imesema, historia itarekodi na kuhukumu mchango mkubwa ya mtu huyu kwa watu na duniani iliyomzunguka.

Trump yeye alitoa taarifa yenye maneno makali akimuita Fidel Castro ni “dikteta dhalimu” ambaye aliwakandamiza watu wake kwa takriban miongo sita. Trump ameahidi kwamba utawala wake utakapoingia madarakani, atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa watu wa Cuba hatimaye wanaweza tena kuanza safari yao kuelekea mafanikio na ukombozi.

Kaka yake marehemu Fidel Castro, Raul castro mwenye umri wa miaka 85 ni rais wa sasa wa Cuba. Amesaidia kurejesha uhusiano na Marekani, lakini hajafanya mageuzi yoyote makubwa ya kisiasa na kiuchumi kwa mfumo wa kikomunisti. Raul Castro anaonekana kuwa katika afya nzuri na mwenye udhibiti kamili. Ameahidi kuachia madaraka mwaka 2018.

Kifo cha kiongozi wa kimapinduzi, Fidel Castro aliyekuwa na umri wa miaka 90, na kuchaguliwa kwa Trump kunaongeza maswali kitu gani kitatokea kwa uhusiano wa Marekani na Cuba. Mshauri mwandamizi wa Trump, Kellyanne Conway amekiambia kituo cha televisheni cha ABC News katika kipindi cha This Week kwamba Trump yuko wazi kwa mipango yoyote ile ya kurejesha uhusiano wa Marekani na Cuba, lakini atataka yawepo makubaliano kwa hilo.

Conway amesema kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa nchini Cuba ni kigezo kikuu cha uhusiano wa siku za baadaye.

Sera za Obama kwa Cuba pia zimekosolewa na wabunge kadhaa kutoka vyama vyote viwili vikuu. Seneta mrepublican Marco Rubio wa Florida ameiita taarifa ya Obama kwa kifo cha Fidel Castro ni ya kusikitisha, akisema hakuna sehemu yoyote inayozungumzia maelfu ya watu aliowaua na aliowafunga gerezani.

XS
SM
MD
LG