Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:54

Crimea yatangaza rasmi kuwa sehemu ya shirikisho la Russia


Kişilər arasında boks (Bakı Kristal Zalı)
Maafisa katika Jamhuri ya Crimea iliyojitenga na Ukraine wanasema wapiga kura kwa idadi kubwa wameidhinisha kujiunga na Russia katika kura ya maoni iliyokuwa na utata ambayo imefanya viongozi wa magharibi kujiandaa na vikwazo dhidi ya Moscow. Jumatatu bunge la Crimea liliidhinisha kura ya maoni, kutangaza uhuru na kuwa rasmi sehemu ya Russia.

Hivi sasa imetangazwa rasmi wa-Crimea tayari wapo chini ya udhibiti wa Russia na wanaiunga mkono Russia wamefanya uchaguzi wa kujitenga kutoka Ukraine na kuungana na Russia. Kufuatia kura ya jumapili ya kujiunga na Russia, bunge la kieneo la Crimea limeomba kuwa sehemu ya shirikisho la Russia.

Lakini nini kinachofuata baada ya kura ya maoni, wote viongozi kwenye peninsula ya Black Sea na dunia waligawanyika katika njia ambazo zinakumbusha mivutano ya enzi ya vita baridi, viko mbali kumalizika.

Wabunge huko Moscow wanaahidi kuweka kando vikwazo vya kisheria ili kuiruhusu Crimea kuingia kwenye shirikisho la Russia. Lakini wasi wasi wa haraka kwa eneo ambalo halina mpaka wa ardhi na Russia unajumuisha usambazaji wake wa nishati, maji na bidhaa nyingine za msingi ambazo hivi sasa wanayapata kutoka Ukraine.

Moscow inatetea hatua ya Crimea kama kuongeza kanuni za kujitambua wenyewe. Mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Russia Vladimir Putin yanaripotiwa kuleta mafanikio kidogo kuziba mwanya uliopo.

Waangalizi wa kigeni walioalikwa na Crimea inayoungwa mkono na serikali ya Russia walitetea kura ya maoni kama inaendeleza kanuni za kimataifa. Mwangalizi kutoka Ubelgiji, Frank Creyelman aliwapuuza wakosoaji wakiwemo kutoka serikali mpya huko Kyiv kwamba upigaji kura ulifanyika kwa mtutu wa bunduki.
XS
SM
MD
LG