Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:06

Upimaji zaidi wa Covid 19 Afrika unaweza kudhibiti maambukizi


Mwanamke na mtoto wake wanamsikiliza mfanyakazi wa afya akielezea utaratibu wa kuchukua sampuli wakati wa upimaji wa virusi vya corona.
Mwanamke na mtoto wake wanamsikiliza mfanyakazi wa afya akielezea utaratibu wa kuchukua sampuli wakati wa upimaji wa virusi vya corona.

Juhudi mpya za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaendelea barani Afrika kutambua haraka maambukizi ya Covid-19 illi kuzuia kusambaa na kudhibiti milipuko zaidi siku za. Usoni kwa ugonjwa huu hatari.

WHO inaripoti zaidi ya kesi milioni 8.4 za Covid-19 Afrika, ikiwemo vifo 214,000. Hata hivyo, tathmini mpya inaashiria kuwa kiwango cha janga katika bara hilo makadario yake yalikuwa ya chini sana.

Tathmini imebaini kuwa ni maambukizi ya Covid-19 moja katika saba yamegunduliwa, ikimaanisha kuwa idadi ya kweli ya kesi huko Afrika huenda ikawa kiasi cha milioni 59. Inakadiriwa kuwa idadi ya chini ya vifo, mmoja kati ya watatu, inaripotiwa.

Hasa ikizingatiwa viwango vya chini vya chanjo katika bara hilo, Mkurugenzi wa WHO kwa Afrika, Matshidiso Moeti anasema ni muhimu sana kufahamu wapi na jinsi virusi vinavyosambaa katika jamii. Hivi sasa, ni asilimia 4.4 ya watu bilioni 1.2 barani humo wamepatiwa chanjo kamili.

Moeti anasema juhudi za WHO za upimaji ni mwelekeo mpya wa haraka, na mmoja mbao ni vyema usaidie kuongeza utambuzi wa viwango kwa kiasi kikubwa.

Anasema WHO inatoa kiasi cha dola milioni 1.8 kwa ajli kuanzisha utekelezaji huo katika nchi nane kama sehemu ya mradi wa majaribio: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Msumbiji, Jamhuri ya Congo, Senegal na Zambia.

Moeti ameonya kuwa sherehe za mwisho wa mwaka huenda zikasababishwa wimbi la nne la virusi vya corona kote Afrika na ulimwenguni.

Ameyasihi mataifa tajiri ambayo yamewapatia chanjo watu wake kiasi cha theluthi mbili kushirikiana hizo dozi hivi sasa na watu huko Afrika, badala ya mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG