Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:04

COVID-19 : Misri kuwachanja wazee na wenye magonjwa sugu


Chanjo ya Sinopham dhidi ya virusi vya corona.
Chanjo ya Sinopham dhidi ya virusi vya corona.

Misri imepanua utoaji wake wa chanjo ya virusi vya Corona Alhamisi kuwajumuisha wazee na watu wenye magonjwa sugu baada ya wiki kadhaa za kuwapa chanjo ya wafanyakazi wa afya, baraza la mawaziri limesema.

Karibu watu 153,000 wameomba chanjo tangu Jumapili wakati nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilipofungua usajili mtandaoni, baraza la mawaziri lilisema katika taarifa.

Misri, nchi ya kiarabu yenye idadi kubwa ya watu duniani ikiwa na zaidi ya milioni 100, imeandaa vituo 40 vya chanjo na ina mpango wa kuongeza idadi ya vituo hivyo baada ya kuwasili kwa chanjo zaidi Waziri Mkuu Mostafa Madbouly alisema.

Misri ilipokea dozi 350,000 za chanjo ya corona iliyotengenezwa na shirila la dawa la China (Sinopharm) kwa shehena mbili tangu mwezi Desemba, pamoja na dozi 50,000 za chanjo iliyotengenezwa na AstraZeneca mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG