Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:55

Baraza la Wawakilishi laidhinisha uchunguzi wa kumuondoa Trump madarakani


Baraza la Wawakilishi lapitisha azimio la uchunguzi wa kumuondoa madarakani Rais Trump Alhamisi, Oct. 31, 2019.
Baraza la Wawakilishi lapitisha azimio la uchunguzi wa kumuondoa madarakani Rais Trump Alhamisi, Oct. 31, 2019.

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha azimio la kuruhusu rasmi uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump unaokusudia kumuondoa madarakani ufanyike.

Azimio hili litawezesha baraza hilo kufanya mahojiano katika vikao na watu mbalimbali ambavyo vitaweza kuonekana na kusikika mubashara na wananchi kupitia vyombo vya habari.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa katika wiki zijazo mashahidi zaidi wataitwa mbele ya kamati ya baraza hilo kutoa maelezo juu ya madai mbalimbali yaliyotolewa dhidi ya Rais Trump.

Hata hivyo Rais amesisitiza kuwa hajafanya makosa yoyote wakati alipozungumza na kiongozi huyo.

Bunge pamoja na mambo mengine itachunguza iwapo kulikuwa na masharti yoyote ambayo Rais aliipa Ukraine, iwapo wanataka msaada wa Marekani uwafikie.

Hatua hiyo inafungua hatua nyingine mpya ya kufanya vikao vya wazi ambapo watu kadha wataitwa mbele ya kamati ya sheria na rais kupata fursa ya kuwa na wakili wa kumtetea mbele ya kamati hiyo. Wajumbe warepublican katika kamati hiyo pia nao watapata fursa ya kuita mashahidi wao wenyewe.

Matokeo ya utaratibu huo yatapelekea hatua ya baraza zima la wawakilishi kupiga kura katika wiki kadha zijazo za kumfungulia mashitaka ya kumwondoa rais madarakani ama la.

XS
SM
MD
LG