Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:23

Congo yaimarisha usalama katika mji mkuu kabla ya michezo ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa


 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi, alipohudhuria Baraza la Haki za Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa huko Geneva.(REUTERS).
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi, alipohudhuria Baraza la Haki za Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa huko Geneva.(REUTERS).

Congo imeimarisha usalama katika mji mkuu Kinshasa huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wa wanamichezo wanaoshiriki katika Michezo ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa inayoanza wiki hii serikali ilisema.

Takriban polisi 4,500 wa ziada wakisaidiwa na wana usalama wa serikali wamepelekwa kabla ya michuano hiyo mratibu wa michezo hiyo Isidor Kwanja, alisema.

Wanamichezo watasindikizwa na polisi na makazi yao yamewekewa Camera za ulinzi.

Ukosefu wa usalama katika jiji hilo ndio kikwazo cha hivi karibuni kwa waandaaji wa michuano ya Jeux de la Francophonie ya siku 10, ambayo tayari ilikuwa imerudishwa nyuma miaka miwili kutoka mwaka 2021 ili kuleta miundo mbinu katika viwango vya kimataifa.

Maafisa wamejitahidi kumaliza viwanja vya mashindano ya riadha, viwanja vya michezo na malazi kwa wakati kwa ajili ya tarehe ya kuanza hapo Ijumaa. Baadhi ya washiriki pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu usalama mjini Kinshasa ambapo uhalifu mdogo mdogo, wizi na utekaji nyara kwa ajili ya fidia ni kawaida.

Forum

XS
SM
MD
LG