Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:27

Upinzani wa Congo kukutana na wawakilishi wa Marekani na EU


mwandamanji nchini Brazzaville, Republic of Congo,

Kiongozi wa upinzani wa vugu vugu la demokrasia na maendeleo la Congo (MCDDI) anasema vya upinzani na makundi ya kiraia, watakutana na wawakilishi wa umoja wa Ulaya na Marekani hii leo ili kuzungumzia hali ya kisiasa nchini humo.

Perfect Kolelas anasema juu katika ajenda itakua ni kuanda mjadala wa kusaidia namna ya kumaliza mzozo huko Congo.

Kolelas aliitaka jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba katiba haikiukwi.

Kolelas amezungumza baada ya polisi kupambana vikali na wafuasi wa upinzani na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanne na wengine wengi kujeruhiwa jana . vijana wa upinzani wanaandamana kupinga juhudi za rais denis soassou nguesso kutaka kutumia kura ya maoni ya jumapili kubadili katiba ili agombaniye mhula mwengine.

XS
SM
MD
LG