Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:06

Mbunge wa upinzani nchini Congo auawa


Wafuasi wa upinzani na polisi wa kupambana na ghasia nchini DRC wakiwafuatilia wapinzani mbele ya ofisi za posta mjini Kinshasa

Mbunge mmoja kutoka chama cha upinzani cha MLC ameuwawa kwa kupigwa risasi mjini Kinshasa nchini Congo

Polisi wa Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo-DRC wanaendelea na uchunguzi kufuatia mauaji ya mbunge mmoja wa upinzani mjini Kinshasa Jumanne jioni, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Jumatatu ijayo.

Mkuu wa polisi mjini Kinshasa Jean de Dieu Oleko, aliliambia shirika la Habari la AFP, kuwa Marius Gangale mbunge wa chama cha Movement for the Liberation of Congo-MLC, ambalo ni kundi kubwa la upinzani katika bunge la nchi hiyo alishambuliwa wakati gari alilopanda liliposimama kwenye msururu wa taa za barabarani Jumanne jioni.

Alisema “tunafanya uchunguzi. Timu moja ya uchunguzi inafanya kazi juu ya kesi hiyo na kutoa ushahidi zaidi wa mwenendo wa hali ya tukio hilo”.
Thomas Luhaka, mbunge mwingine wa chama cha MLC, alisema mbunge huyo alikuwa ndani ya gari lake akiwa na mke wake wakati waliposhambuliwa katika uhalifu uliofanywa kwenye eneo la jirani.

Alisema “watu wawili walijaribu kufungua mlango wa nyuma wa gari lake ili waingie lakini walishindwa kwa sababu milango ilikuwa imejifunga yenyewe kwa ndani. Mtu mmoja kati ya washambuliaji hao alitoa silaha yake na kumfyatulia risasi mbunge huyo”.

Hakukuwa na matamshi ya haraka kwamba mauaji hayo yalihusiana na sababu za kisiasa, lakini Luhaka alisema alikuwa na sababu ya kufikiri hivyo kuwa tukio hilo lilihusiana kabisa na uhalifu wa kisiasa.

Alisema “tunajiuliza maswali. Tayari tulishapoteza naibu wa chama chetu mjini Kinshasa miaka mitatu iliyopita, ambapo aliuwawa na watu wenye silaha wakati alipokuwa akisindikizwa na walinzi wake, akifananisha tukio hili na Makamu Rais wa zamani mjini Kinshasa, Daniel Botethi.

Uchaguzi mkuu wa Jumatatu katika taifa hilo la Afrika ya kati umegubikwa na ghasia baina ya wafuasi wa Rais Joseph Kabila na wale wa makundi ya upinzani.

XS
SM
MD
LG