Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Mshauri wa Kabila akanusha kumtafuta ubaya Katumbi Chapwe


FILE - Moise Katumbi Chapwe, Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Juni 2, 2015 in Lubumbashi.
FILE - Moise Katumbi Chapwe, Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Juni 2, 2015 in Lubumbashi.

Mshauri mkuu wa rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekanusha taarifa kuwa utawala huo umeanza njama za kumtafuta kwa ubaya kiongozi wa upinzani Moise Katumbi Chapwe ambae ni mfanya biashara wa kimataifa aliyenuia kugombea urais kwenye uchaguzi ambao bado haujaamuliwa kama utafanyika.

Katumbi yuko Marekani kwa matibabu ambapo imeripotiwa kuwa amekuwa akikutana na viongozi wa ngazi za juu hapa mjini Washington.

Mshauri huyo mkuu wa kidiplomasia wa rais Kabila, Kikaya Bin Karubi amesema Serikali yake haina tatizo na kiongozi huyo wa upinzani kufanya mikutano hapa Washington au popote pale duniani. Tatizo pekee tulilo nalo ni kwamba ameaga anakwenda kutibiwa ana kesi Congo na aliambiwa asiseme lolote akiwa nje ya nchi kuhusiana na kesi hii kwa hiyo anaweza kukutana na watu na kuzungumza alimradi asizungumzie kesi hatuna tatizo lolote alisema Karubi.

Mwezi uliopita, Katumbi alihukumiwa kifungo cha miaka 3 jela ambayo wachambuzi wanasema itamzuia kuwania wadhifa wa rais. Wafuasi wake wanasema kuwa serikali inamuandama kwa kuwa ndiye kiongozi wa upinzani pekee mwenye uwezo wa kupingana na rais Kabila.

XS
SM
MD
LG