Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:02

Wakongo wakimbia mapigano na kuingia Rwanda


Wakimbizi kutoka Congo wakiwa katika kambi ya Nkamira Transit nchini Rwanda
Wakimbizi kutoka Congo wakiwa katika kambi ya Nkamira Transit nchini Rwanda

Mapigano makali yanaendelea katika mkoa wa Masisi nchini DRC kati ya wanajeshi waasi na jeshi la Serikali

Raia wengi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanakimbia mapigano katika maeneo yao na kuelekea katika nchi jirani ya Rwanda.

Mkazi mmoja katika eneo la mashariki ya DRC ambako mapigano hivi sasa yanaendelea, Annie Kabeja mwenye umri wa miaka 34 alisema wakati milio ya risasi iliposikika katika eneo analoishi, aliungana na wimbi la maelfu ya wakongo na kuondoka katika eneo ambapo alitembea kwa muda wa siku mbili akiwa na mtoto wake hadi kuingia nchini Rwanda.

Bi.Kabera akiwa na mtoto wake mdogo mgongoni, alisubiri kwenye mstari mrefu pamoja na wakongo wengine kwenye kambi ya wakimbizi ya Nkamita Transit kupokea mgao wa chakula na mahitaji mengine ya msingi.

“Tulisikia milio ya risasi na milipuko. Tulikuwa hatuna uamuzi wa kufanya isipokuwa kukimbia kutoka eneo hilo hadi eneo jingine na baada ya kuwasili nchini Rwanda, hatukuweza kulala, risasi zilikuwa zikiruka kila mahali.”

Mapigani huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC yamezidi baada ya darzeni ya wanajeshi waasi siku ya Jumatatu kuunda kundi jipya katika eneo kubwa ambalo waasi wengi walianzia huko.

Kundi hilo jipya liliundwa na wanajeshi waasi wanaojiita March 23, ikiwa ni tarehe katika mkataba wa amani wa mwaka 2009 uliotiwa saini na makundi ya uasi na serikali ya Congo. Kundi hilo linaongozwa na Kanali ambaye zamani alikuwa chini ya Bosco Ntaganda, mbabe wa kivita wa zamani ambaye aliingia katika jeshi la Congo chini ya mkataba wa amani licha ya kutafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.

Msemaji wa jeshi la Congo, Kanali Sylvain Ekenge aliliita kundi jipya ni ‘bandia’ lakini mapambano kati yao na jeshi la Congo yaliendelea kwa siku kadhaa katika mkoa wa Masisi uliopo Kivu Kaskazini.

Rwanda kwa kawaida hutumia sehemu katika milima ya Rwanda, kuwakaribisha kwa muda wakimbizi kutoka Congo.

Straton Kamanzi meneja wa kambi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa alisema kambi hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua wakimbizi 4,000 lakini hivi sasa ina nyumba 7,000. Wanawake, wasichana na watoto wadogo wanalala chini pamoja kwenye makazi ya muda.

Richard Ndaula ambaye anafanya kazi na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa alisema kati ya watu 250 na 300 wanajitokeza kwenye kambi hiyo iliyopo karibu na mpaka na Congo kila siku.

XS
SM
MD
LG