Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 03:56

Watu 27 wanasadikiwa kupoteza maisha katika ajali ya boti Congo


Wanawake wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Wanawake wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Watu 27 wanasadikiwa kupoteza maisha katika ajali ya boti ambayo imetokea kwenye ziwa maindombe kwenye jimbo la Bandundu mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya congo.

Kwa mujibu wa radio okapi ya umoja wa mataifa boti mbili ziligongana na moja ikapinduka na hivyo kusababisha vifo hivyo. Naibu Gavana wa Maindombe, Massamba Malika, ameiambia radio okapi kwamba boti hizo mbili zilikuwa zinasafiri katika njia tofauti kati ya ingongo na bokoro na katika hali ya kuepuka ukungu uliokuwa umetanda, ziliamua kubadili njia na hivyo kugongana.

Amesema miili ya watu hao 27 bado iko kwenye ziwa maindombe, na huenda kuna abiria wengine zaidi ambao wamepoteza maisha. Ajali ilitokea Jumamosi usiku muda ambao boti zinashauriwa kutofanya safari ili kuepuka ajali. Malika amesema bado haiko bayana watu wangapi walikuwa katika boti, lakini hawakuzidi watu 100. Timu ya uokozi imekwenda katika eneo la ajali ili kujaribu kuipata miili ya watu hao.

December mwaka jana watu 18 walifariki na wengine 70 kupotea baada ya ajali kutokea katika ziwa hilo hilo.

XS
SM
MD
LG