Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 07:21

Colonial Pipeline yaahidi kurejesha tena huduma za mafuta Marekani


Upungufu wa mafuta ya gari umeshuhudiwa nchini Marekani

serikali ya Marekani na maafisa wanaohusika na kitengo cha mafuta nchini humo wanawasihi waendeshaji magari kuondoa hofu ya kununua gesi na kuweka nyingine kama akiba kwa kuhofia upungufu wa mafuta unaoshuhudiwa hivi sasa

Mwendeshaji wa bomba kuu la mafuta Colonial Pipeline nchini Marekani, lililoathiriwa na shambulizi hadi kwenye mfumo wake wa kompyuta ametangaza kuanza tena shughuli za usambazaji mafuta.

Colonial Pipeline ilisema kuanza tena shughuli zake Jumatano lakini itachukua siku kadhaa kwa mlolongo wa uzalishaji wa bidhaa kurejea katika hali ya kawaida. Masoko kadhaa yanayohudumiwa na Colonial Pipeline huwenda yakashuhudia, au kuendelea kushuhudia usumbufu wa huduma wakati wa kipindi cha kurejea hali ya kawaida.

Kampuni ya mafuta Colonial Pipeline katika kituo chake huko Pelham, Alabama.
Kampuni ya mafuta Colonial Pipeline katika kituo chake huko Pelham, Alabama.

“Colonial itasambaza gesi, dizeli na mafuta ya ndege kwa usalama kadri iwezekanavyo, na itaendelea kufanya hivyo hadi masoko yarejee katika hali ya kawaida” taarifa ilieleza.

Wakati huo huo serikali ya Marekani na maafisa wanaohusika na kitengo cha mafuta nchini humo wanawasihi waendeshaji magari kuondoa hofu ya kununua gesi na kuweka nyingine kama akiba kwa kuhofia upungufu wa mafuta unaoshuhudiwa hivi sasa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG