Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:33

Kinywaji cha kahawa kinapata umaarufu zaidi Afrika Kusini


Kahawa
Kahawa

Mandhar ya kahawa inazidi kushamiri nchini afrika kusini ikisukumwa na watu wanaopenda kinywaji cha kahawa, mbegu bora za kahawa na uwelevu kuhusu asili ya zao hilo ambalo ni mojawapo ya kinywaji maarufu sana duniani.

Miaka mitano ilopita , sauti ya kahawa ikitengenezwa kutoka kwenye mbegu safi za kahawa Ilikuwa ni sauti ngeni kwa Jermina Kgole.

Kgogle anasema, alikuwa akinywa kahawa ambayo ilikuwa imeshasagwa, kama vile Ricofee, Nescafe na sikuweza hata kuelezea tofauti zao.

Lakini sasa wakati umebadilika. Kgogle sasa ni mhudumu wa juu wa kahawa katika moja ya maduka bora yanayouza kahawa mjini Johannesburg, na ni miongoni mwa mapinduzi ya kahawa yanayofanyika nchini Afrika kusini.

coffee
coffee

Biashara ya kahawa inashamiri katika uchumi mkubwa wa barani Afrika. Shirika la utafiti wa soko la Insight survey likielezea kuwa maduka ya kahawa yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha miaka 2 ilopita kwa ongezeko la takriban asli mia 7 katika mapato.

Zaidi ya waafrika kusini millioni 19 ambao ni Zaidi ya theluthi moja ya idadi ya watu huko, wanategemea kunywa japo kikombe kimoja cha kahawa kila siku. Na kwa kila kikombe cha kahawa wauzaji kahwa wanajaribu kuwavutia wapenda kahawa waondokane na kahawa ambayo ni ile ya kutengeneza mara moja maaruf kama instant coffee.

Hilo limedhihirishwa katika foleni zilokuwepo baada ya kufunguliwa hivi karibuni kwa duka kubwa la kuuza kahawa la starbucks mjini Johannesburg. Waafrika kusini wa rangi zote walisubiri kwa uvumilivu kwa saa kadhaa wakisubiri kupata kahawa katika vikombe vyao vya rangi ya kijani na nyeupe.

Lakini mfanyabiashara wa kahawa Wayne Burrows wa Urban Grind mjini johanesburg anasema kizazi kipya cha wanywaji kahawa Afrika kusini kinahamu zaidi ya kutaka kujuwa kil kilichopo ndani ya kikombe chao, na kimetokea wapi.

Anasema hilo ndilo linaifanya mapinduzi ya kahawa ya Afrika kusini kuwa tofauti.

Burrows anasema, anataka kumjuwa mkulima aliyevuna kahawa hii, mkulima aliyeitengeneza ili niweze kumelezea mteja wa kahawa anaekunywa kahawa. Na hili linatokea kwa sababu mteja anataka kufahamu zaidi kuhusu kahawa. Wanataka kuielewa kahawa nzuri. Amini au usiani, wanauliza maswali tofauti kuhusu kahawa . Na hili ni wimbi jipya linalotukumba.

Bi Kgogle anasema hali imebadilika kwa sababu watu weusi sasa wanaanza kunywa kahawa na wanaipenda.

XS
SM
MD
LG