Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:57

CODECO na ADF wameua raia huku M23 wakiendelea kudhibithi sehemu kadhaa DRC


Mazishi ya raia waliouawa katika mashambulizi ya makundi ya waasi karibu na kambi ya wakimbizi ya Plain Savo, kaskazini mashariki mwa DRC, Feb 4, 2022
Mazishi ya raia waliouawa katika mashambulizi ya makundi ya waasi karibu na kambi ya wakimbizi ya Plain Savo, kaskazini mashariki mwa DRC, Feb 4, 2022

Watu 32 wameuawa kutokana na mashambulizi ya makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa umoja wa mataifa Stephene Dujaric amesema waliouawa ni raia wa mkoa wa Ituri.

Watu 20 waliuawa na waasi wa kundi la CODECO huku darzeni yaw engine wakiuuawa na waasi wa Allied democratic forces ADF.

Dujarric amesema kwamba hali mashariki mwa DRC ni ya kuchanganyikiwa na ngumu kwa walinda usalama wa umoja wa mataifa kupata taarifa za kutosha.

Mapigano kati ya kundi la waasi la CODECO kutoka kundi la kikabila la Lend una kundi la Zaire kutoka kabila la Hema yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 2017 na yameongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Desemba, umoja wa mataifa ulisema kwamba makundi ya waasi yanaendelea kupanuka kwa ukubwa na kushikilia sehemu kadhaa, yakishambuia rai ana jeshi la serikali, huku yakitoza raia ushuru katika sehemu wanayoshikilia.

Mauaji hayo yametokea wakati ghasia zinaendelea kuongezeka mashariki mwa DRC ambapo kuna zaidi ya makundi ya waasi 120 yanayopigana kudhibithi sehemu kadhaa za ardhi, madini na baadhi kulinda jamii zao.

Hali imeendelea kuwa mbaya katika jimbo la Kivu kaskazini ambapo kundi la waasi la M23 linaendelea kudhibithi sehemu kadhaa za nchi.

Waasi hao wanadhibiti miji ya Masisi na Sake, ambapo zaidi ya watu 65,000 wamelazimika kutoroka makwao kutokana na mapigano.

XS
SM
MD
LG