Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 23:07

Clinton aongoza katika uchunguzi mpya wa maoni.


Mdemokrat Hillary Clinton akisalimiana na wafuasi wake huko Akron, Ohio, Okt. 3, 2016.
Mdemokrat Hillary Clinton akisalimiana na wafuasi wake huko Akron, Ohio, Okt. 3, 2016.

Taarifa mpya ya ukusanyaji maoni katika kampeni ya urais wa Marekani inaonyesha mdemokrat Hillary Clinton amechukua tena uongozi dhidi ya Mrepublikan Donald Trump tangu mdahalo wao wa kwanza ambapo wapiga kura wengi wanafikiri ameshinda.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha Clinton waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani akiongoza dhidi ya tajiri wa nyumba anayegombea kwa mara ya kwanza na wagombea wengine wawili, mgombea binafsi Gary Johnson na mgombea wa chama Green Party Jill Stein .

Uchunguzi mwingine wa maoni unaonyesha majimbo yenye ushindani yaliofanya uchunguzi wao baada ya mdahalo wiki iliyopita ulionyesha Clinton akipata uongozi dhidi ya Trump. Uchaguzi wa Marekani mshindi hachaguliwi kwa kura za watu wengi bali ni kutokana na ushindi wa majimbo 50 yaliopo huku majimbo yenye watu wengi yakiwa na kura zaidi na kutoa maamuzi ya mshindi wa jumla kwenye uchaguzi.

XS
SM
MD
LG