Seneta Bernie Sanders ameibuka mshindi katika jimbo la Oregon huku Bi Hillary Clinton akishinda kura ya awali kwenye jimbo la Kentucky.
Clinton aliongoza dhidi ya seneta wa Vermont, Bernie Sanders kwa zaidi ya kura 2,000 kwenye uchaguzi huo uliofanyika Jumanne.
Warepublican walifanya uchaguzi wao katika jimbo la Kentucky mwezi Machi na ushindi ulikwenda kwa Donald Trump mgombea anayetarajiwa hivi sasa kupata uteuzi wa kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi mkuu.
Clinton bado ana idadi kubwa ya wajumbe hadi hivi sasa licha ya Sanders kupata ushindi katika majimbo kadhaa na kuapa kuendelea kubaki katika kinyang’anyiro hiki cha kuwania uteuzi wa chama hadi kufikia mkutano mkuu wa wajumbe wa Democrat unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai katika jimbo la Philadelphia.
Facebook Forum