Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:21

Bi Clinton aukaribia ugombea urais


Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hilary Clinton, jana alipata uteuzi wa kuwania urais wa Marekani na kuwa mwanamke wa kwanza kuwakilisha chama kikubwa cha kisiasa, katika kinyang’anyiro cha kutaka kuingia kwenye Ikulu ya Marekani.

Mpinzani wake kwenye chama cha Demokratik, na ambaye ni Seneta wa jimbo la Vermont, Bernie Sanders, alishinda kwenye jimbo la North Dakota, lakini Clinton akamshinda kwenye uchaguzi wa awali wa South Dakokta, New Mexico na New Jersey.

Rais Barack Obama aliwapigia simu wagombea hao wawili jana Jumanne.

Obama alimpongeza Clinton kwa kupata idadi ya kuwajumbe wanaohitajika ili kupata uteuzi huo, na pia kumshukuru Sanders kwa kuwahamasisha mamilioni ya Wamarekani kuhusu umuhimu wa kupambana na ukosefu na usawa kiuchumi.

Sanders aliwaambia wafuasi wake katika jimbo la California kwamba alimpigia simu Bi Clinton na kumpongeza kwa ushindi wake.

Lakini ingawa alizungumza kuhusu kufanya kazi pamoja na Clinton ili kumshinda mgombea wa Republikan, Donald Trump, Sanders hakuonekana kukiri kwamba ameshindwa na Waziri huyo wa zamani, na aliapa kuendelea na mapambano.

XS
SM
MD
LG