Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:54

Clinton anakaribia kupata uteuzi wa Democrat aweze kuwania urais


Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton akizungumza huko California. Mei 27, 2016.
Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton akizungumza huko California. Mei 27, 2016.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton anakaribia uteuzi wa Democratic kuwania urais lakini anakabiliwa na mtihani wa mwisho huko California, jimbo lenye watu wengi dhidi ya mpinzani wake pekee, seneta wa Vermont, Bernie Sanders.

Clinton anaangazia kuwa mwanamke wa kwanza Rais wa Marekani na anakaribia kabisa kupata wingi wa wajumbe kwa ajili ya mkutano mkuu wa chama mwezi Julai ambao utateua mgombea urais.

Hivi sasa ana wajumbe 2,383 anaohitaji na kuwa mgombea wa kwanza mwanamke kuwania urais kutoka katika moja ya vyama vikuu vya siasa Marekani. Sanders ana ahadi za wajumbe 1,542.

Clinton mwanadiplomasia wa juu kutoka mwaka 2009 mpaka 2013 huenda akapata uteuzi hapo Juni saba hili litatokea wakati California bado wakipiga kura wiki ijayo. majimbo manne ambayo wiki ijayo yatafanya uchaguzi wa awali ni Montana, New Mexico, North Dakora na South Dakota, lakini California ndiyo lenye idadi kubwa ya wajumbe na kumvutia zaidi Clinton.

XS
SM
MD
LG