Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:18

CIA yazungumzia operesheni ya kumuua bin Laden


Aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaida, Osama bin Laden.
Aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaida, Osama bin Laden.

Idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA) imetoa habari kupitia ukurasa wake wa Twitter kuhusu jinsi operesheni ya shambulizi lililomuuwa kiongozi wa ugaidi lilivyofanyika kupelekea maelfu ya watu kujibu na kurudia Tweet hiyo ikionekana imependwa na waunga mkono huku wengine wakijibu kwa kukosoa mpaka kutukana.

Operesheni hiyo ilipewa kibali na Rais Barack Obama Mei 2011 ikihusisha vikosi maalum kwa kuingia kwenye nyumba yake huko Abotabad, Pakistan kwa kutumia helikopta na baadaye kuutupa mwili wa Osama Bin Laden baharini.

Twitter imekuwapo tangu 2006 lakini CIA imejiunga na mtandao huo miaka miwili tu iliyopita. Tweet za mtandao huo zipatazo 1,600 zinazungumzia historia ya idara hiyo, wasifu wa wafanyakazi waliouwawa kazini au maelezo kwa umma yanayotolewa na maafisa wanaofanyakazi hivi sasa .

XS
SM
MD
LG