Mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu wa kiraia nchini Mali, Choguel Kokalla Maiga amerudishwa kizuizini na atafikishwa mahakamani mwezi Julai, chanzo cha mahakama kimesema Jumanne, baada ya vuguvugu lao la kisiasa kuwakosoa waziwazi watawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Vuguvugu la M5-RFP siku ya Ijumaa lilitoa tamko kali dhidi ya makanali waliotwaa madaraka mwaka 2020 na kurefusha zaidi utawala wao baada ya kushindwa kuweka tarehe ya mwisho ya mwezi Machi ya kuandaa uchaguzi, na kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.
Boubacar Traore ambaye alitia saini taarifa hiyo alikamatwa siku ya Jumatatu. Mjumbe mmoja katika msafara wake alisema alichukuliwa na maafisa wa ujasusi kutoka ofisini kwake katika jengo lenye makaazi ya huduma za waziri mkuu.
Amewekwa kizuizini kwa kuharibu nchi, kuidharau mahakama, kuvuruga utaratibu wa umma, kuchapisha uongo kutoka Mahakama ya Bamako, kimesema chanzo ambacho hakikutaka jina lake litajwe. “Kesi yake imepangwa kusikilizwa Julai Mosi”, kilisema chanzo hicho.
Forum